Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, marehemu Ayatullah Alawi Gorgani katika moja ya hotuba zake kwa mnasaba wa siku za Fa'timiyya, ameashiria mada ya “Bibi Zahraa kama chanzo cha uongozi wa kiwilaya na unabii”, mada ambayo inawasilishwa kwenu kama ifuatavyo:
Mzizi wa “Wilaya” na “unabii” unapatikana kupitia mkono mtukufu wa Bibi Fatima Zahraa (s.a).
Ndiyo maana Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) kuhusu yeye amesema: «فاطمه اُمّ أبیها» “Fatima ni mama wa baba yake”; yaani mama wa baba yake mwenyewe.
Tamko hili ni la kina sana. Maana yake ni kwamba lau isingekuwa uwepo wa Bibi Zahraa (s.a) na watoto wake wakubwa wenye heshima, basi kusingelibakia chochote katika dini ya Uislamu. Kubakia kwa dini ya Mtume (s.a.w.w.) na kuendelea kwake hadi zama za Imam Mahdi (a.t.f.s.) ni kwa baraka ya uwepo wa Bibi Zahraa (s.a) na kizazi chake kitoharifu.
Kwa hivyo, Bibi Zahraa (s.a) anayo nafasi kubwa mno na daraja lisilo na mfano. Utukufu na adhama yake umefikia kiwango ambacho Mtume wa Mungu (s.a.w.w.) alimuita “mama wa baba yake”.
Kwa nini tamko hili limetumika? Kwa sababu neno “umm” katika Kiarabu lina maana ya asili na mzizi; kama vile wanavyoita mji wa Makka “Ummul-Qura”, kwa kuwa asili ardhi imejengeka kutoka hapo.
Basi, kama vile Makka ni chanzo cha uumbaji wa ardhi, vivyo hivyo Bibi Zahraa (s.a) ni mzizi na chanzo cha Wilaya na Unabii ulimwenguni.
Kutokana na tamko hili “Ummu Abiiha”, tunaweza vyema kutambua ukubwa na cheo cha adhama ya Bibi.
Matarajio yetu kutoka kwa ndugu na dada wote waumini ni kwamba waheshimu siku za Fa'timiyya, waziadhimishe kwa heshima na taadhima, wajitahidi katika kuandaa majlisi za maombolezo na majonzi ya Bibi Zahraa (s.a), na kadiri ya uwezo wao, wajitahidi katika kutekeleza haki yake.
Kwa sababu haki ya Bibi Zahraa (s.a) kwa kweli haiwezi kulipwa kikamilifu, lakini kadiri ya uwezo wetu lazima tufanye.
Kwa nyinyi wote waombolezaji wa Bibi Zahraa (s.a) ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape thawabu inayofaa na stahiki, na kutoka kwa Mwenyezi Mungu naomba atukubalie dua yetu kwa baraka za Bibi Zahraa (as), na atuhesabu miongoni mwa wasaidizi wa uwepo wake mtukufu na wa mwanawe mkubwa, Imam wa Zama (a.t.f.s.).
Maoni yako